Prof. Mohamed H. Abdulaziz Atuzwa!
PDF version
Date and time: 
Wed, 2016-09-28 15:01
Location / Venue: 

RISSEA, Mombasa

Prof. Abdulaziz akipokea zawadi kutoka kwa Prof. Kimani Njogu aliyempokeza kwa niaba ya CHAKITA na Twaweza Communications akisaidiana na Prof. Sangai Mohochi, Mwenyekiti wa CHAKITA Dkt. Kalandar Khan, Mkurugenzi wa RISSEA.

Mnamo tarehe 8 na 9 Septemba  wataalam wa Kiswahili walijumuika jijini Mombasa kumwenzi "mlezi" wao Prof. Mohamed Hassan Abdulaziz. Profesa Abdulaziz alimiminiwa sifa kutokana na kazi aliyoifanya kukuza Kiswahili kwa muda usiopungua miaka sitini. Sherehe hiyo ilijumuisha kongamano lililofunguliwa na Gavana wa Mombasa Hassan Joho na kutamatishswa na Prof. Inyani Simala ambaye ni Katibu Mtendaji wa  Katibu Mkuu, Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Zanzibar. Mkuu wa Chuo cha Sanaa katika Chuo Kikuu cha Nairobi pia alitoa hotuba ambayo ilisomwa kwa niaba yake na Makamu Mkuu wa Kitivo cha sanaa Prof. Rayya Timammy. Baadhi ya wasomi tajika wa Kiswahili waliohudhuria ni pamoja na Prof. M. M. Mulokozi kutoka Tanzania na Prof. Rocha Chimerah. Hotuba maalum ilitolewa na Prof. Okoth Okombo nazo habari kumhusu Prof. Abdulaziz zikasomwa na Prof. John Habwe na Mkuu wa Idara Prof. Iribe Mwangi. Kongamano hilo liliandaliwa na CHAKITA kwa ushirikiano na Twaweza Communications

Wahadhiri wa Idara ya Kiswahili: kutoka kushoto, Dkt. Mwaliwa, Dkt. Mukhwana, Prof. Rayya, mwenyewe Prof. Abdulaziz, Prof. Iribe, Mw. Mungania, Prof. Kineene na Prof. Habwe

Prof. Okoth Okombo aliyetoa hotuba maalum, pamoja na Prof. Kineene na Dkt Mwaliwa

Baadhi ya waliohudhuria wakifuata mawasilisho.

Expiry Date: 
Wed, 2022-09-28 15:01