Mkataba wa Utoaji Huduma

Idara ya Kiswahili  ina wajibu wa  kufundisha na kufanya utafiti pamoja na kuratibu shughuli za masomo na ufundishaji wa fasihi na isimu katika Chuo Kikuu cha Nairobi.   Ni matumaini yetu kuwa juhudi hizi zitakuwa na ufanisi mzuri katika nchi  Kenya.

Mkataba huu wa huduma una malengo ya kubainisha wajibu wetu ni upi na jinsi tunalenga kutoa huduma zetu kwa wateja wetu. Unabainisha uhusiano wetu  na mtagusano tunaolenga kuwa nao kati yetu na umma wa Kenya pamoja na ulimwengu kwa ujumla.  

Tutahakikisha kuwa mkataba huu wa huduma unaboreshwa ili kuweza kuafikiana na kutumika kulingana na kanuni za kijumla za Chuo Kikuu cha Nairobi.

WAJIBU WETU

 • Kufanya utafiti katika isimu na fasihi 
 • Kutoa mafunzo ya hali ya juu
 • Kutoa ushauri kwa wasomi
 • Kutafuta ushirikiano na asasi zingine za ulimwengu katika utafiti 
 • Kuchapisha matini za kufundishia 
 • Kutumia matokeo ya tafiti zilizofanywa katika ufundishaji
 • Kuchapisha bunilizi za Kiswahili 
 • Kutoa huduma za tafsiri 

WATEJA WETU 

 • Wananchi  na watu wote wanaoishi nchini Kenya  
 • Asasi zote za umma na za kibnafsi    
 • Wanafunzi 
 • Wazazi  
 • Watafiti  
 • Wasomi wanazueu nchini 
 • Washirika wetu katika maendeleo
 • Asasi zingine zamasomo na  ufundishaji 

AHADI ZETU KWA WATEJA

 • Kutoa huduma kwa wakati
 • Kuruhusu mapendekezo na kukosolewa  
 • Kufanya kazi kulingana na sera na kanuni za chuo 
 • Kutumia raslimali kikamilifu  
 • Kutoa huduma bora  
 • Kuhudumu kwa njia ya uadilifu na kitaaluma 
 • Kutoa mazingira bora ya  ufundishaji na utafiti 

 

HUDUMA ZETU 

 • Kutoa mafunzo  kwa wafanyikazi
 • Kutoa ushauri kwa wasomi wachanga 
 • Kufanya utafiti 
 • Kusahihisha na kutathmini 
 • Uhariri 
 • Kuchapisha na kutoa mawaidha katika masuala ya lugha 
 • Kusawazisha viwango vya  masomo  

 

KUSULUHISHA MALALAMISHI  

Wateja wetu wanashauriwa kuwasilisha  mamalamishi yao kwa kufuata njia zifuatazo:

 • Ana kwa ana
 • Kupiga simu
 • Baruapepe
 • Barua
 • Kisanduku cha mapendekezo

Idara itadumisha usiri wa mawasiliano yote baina yake na mteja

WAJIBU WA MTEJA 

 • Kupata huduma bora 
 • Kutagusana na idara kwa njia ya kunufaishana
 • Kukosoa kwa nia ya kutaka kuboresha ubora wa huduma
 • Kuleta majibu kuhusiana na ubora wa huduma zinazotolewa 
 • Kushiriki katika shughuli za idara  
 • Kupiga ripoti kwa haraka pale kasoro zinapobainika
 • Kupeana taarifa za kutosha ili kuwezesha usaidizi kupatikana

 

KUJITOLEA KWETU KWA UTOAJI WA HUDUMA

 • Wafanyikazi watawezeshwa kwa mujibu wa sera na sharia za Chuo Kikuu cha Nairobi
 • Idara ya Kiswahili itabuni njia za kutolea malalamiko na kuulizia
 • Usahihishaji utakamilika kwa muda wa majuma mawili kulingana na matakwa ya chuo 
 • Ufundishaji utaanza kwa wakati unaofaa
 • Ufundishaji wote utatekelezwa kulingana na ratiba za Chuo Kikuu cha Nairobi
 • Ufundishaji wote utalingana na silabasi mbalimbali zilizoidhinishwa na seneti
 • Idara itahakikisha ya kwamba inakumbatia teknolojia 
 • Kesi zote za kinidhamu miongoni mwa wanafunzi zitakabidhiwa kwa mamalaka makuu ya kinadhamu kwa wakati unaofaa 
 • Ratiba za masomo zitawekwa wazi katika hadhara kwa wote kuona  
 • Tutahakikisha kuwepo kwa mawasiliano mema baina ya Idara ya Kiswahili, kitivo, shule na mamlaka makuu ya chuo 
 • Huduma zote katika idara zitaongozwa na sharia zilizowekwa na Chuo Kikuu cha Nairobi