Latest News & Announcements

Hongera Profesa Mwangi kwa Kutambuliwa na Rais

Prof. Iribe Mwangi, mwalimu wa Kiswahili ni miongoni mwa Wakenya 460 waliotuzwa na Rais William Ruto katika sherehe za Kitaifa za 59 za jamuhuri. 

Profesa Iribe ni ni mwenyekiti wa Idara ya Kiswahili chuo kikuu cha Nairobi. Aliweza kutunukiwa tuzo ya Head of State Commendation (HSC) kwa mchango wake katika makuzina maendeleo ya Kiswahili ambayo yameathiri sera ya lugha nchini Kenya.

TANZANIA YAANZISHA DARASA LA KWANZA LA KISWAHILI NCHINI MALAWI

Darasa la Kiswahili Nchini Malawi ni sehemu ya Jitihada za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ubalozi wake Nchini Malawi kukipeleka kiswahili nje kama Lugha, utamaduni na bidhaa. Darasa la kwanza limeendeshwa na Wataalam wa kiswahili kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na baadaye darasa hilo litaendelezwa kwa ushirikiano kati ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Chuo Kikuu cha Hebron cha Nchini Malawi.

 

Bunge la kitaifa lajadili uwepo wa baraza la kiswahili

Wabunge wanasema ni wakati kwa Kenya kubuni baraza la kitaifa la kiswahili, kusaidia kuipa lugha hii hadhi inayostahiki. Wabunge waliokuwa wakichangia hoja ya mbunge wa Kamukunji Yusuf Hassan walisema kuwa, kuimarishwa kwa utumizi na hadhi ya kiswahili kutasaidia kuimarisha utangamano zaidi, sio tu hapa nchini na kanda ya Afrika Mashariki, bali pia dunia nzima ambapo lugha hii inaenziwa.