UoN @50

UoN@50

Kuanzia mwezi Juni 2020 hadi Juni 2021, Chuo Kikuu cha Nairobi kinaadhimisha miaka 50 tangu kuasisiwa kwake. Kumekuwa na shughuli nyingi hasa webina za kiusomi ambazo zimekuwa zikiendelea na zitaendelea hadi Juni 2021. Idara ya Kiswahili tayari imekwishaandaa webina iliyokuwa na kaulimbiu ya “Kiswahili Ulimwenguni.” Hata hivyo, kilele cha sherehe hizi kitakuwa Alhamisi tarehe 10 Desemba 2020 kuanzia saa nane alasiri. Balozi Simon Nabukwesi ambaye ni Katibu Mkuu wa Idara ya Elimu ya Vyuo Vikuu katika Wizara ya Elimu atatoa hotuba katika hafla hiyo kama mwakilishi wa Serikali ya Kenya. Mgeni mashuhuri wa sherehe hiyo ni Dkt. Manu Chandaria ambaye atatoa hotuba yake kwa njia ya mtandao.

Sherehe hizo za UoN@50 zitapeperushwa moja kwa moja kupitia YouTube, Facebook na tovuti ya Chuo Kikuu cha Nairobi www.uonbi.ac.ke.

Tafadhali bonyeza kwenye kiungo hiki ili ufuatilie sherehe hizo:  https://youtu.be/1dvj-o3ROKs