Idara ya Kiswahili ina wajibu wa kufundisha na kufanya utafiti pamoja na kuratibu shughuli za masomo na ufundishaji wa fasihi na isimu katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Ni matumaini yetu kuwa juhudi hizi zitakuwa na ufanisi mzuri katika nchi Kenya.
Mkataba huu wa huduma una malengo ya kubainisha wajibu wetu ni upi na jinsi tunalenga kutoa huduma zetu kwa wateja wetu. Unabainisha uhusiano wetu na mtagusano tunaolenga kuwa nao kati yetu na umma wa Kenya pamoja na ulimwengu kwa ujumla.
Tutahakikisha kuwa mkataba huu wa huduma unaboreshwa ili kuweza kuafikiana na kutumika kulingana na kanuni za kijumla za Chuo Kikuu cha Nairobi.
WAJIBU WETU
- Kufanya utafiti katika isimu na fasihi
- Kutoa mafunzo ya hali ya juu
- Kutoa ushauri kwa wasomi
- Kutafuta ushirikiano na asasi zingine za ulimwengu katika utafiti
- Kuchapisha matini za kufundishia
- Kutumia matokeo ya tafiti zilizofanywa katika ufundishaji
- Kuchapisha bunilizi za Kiswahili
- Kutoa huduma za tafsiri
WATEJA WETU
- Wananchi na watu wote wanaoishi nchini Kenya
- Asasi zote za umma na za kibnafsi
- Wanafunzi
- Wazazi
- Watafiti
- Wasomi wanazueu nchini
- Washirika wetu katika maendeleo
- Asasi zingine zamasomo na ufundishaji
AHADI ZETU KWA WATEJA
- Kutoa huduma kwa wakati
- Kuruhusu mapendekezo na kukosolewa
- Kufanya kazi kulingana na sera na kanuni za chuo
- Kutumia raslimali kikamilifu
- Kutoa huduma bora
- Kuhudumu kwa njia ya uadilifu na kitaaluma
- Kutoa mazingira bora ya ufundishaji na utafiti
HUDUMA ZETU
- Kutoa mafunzo kwa wafanyikazi
- Kutoa ushauri kwa wasomi wachanga
- Kufanya utafiti
- Kusahihisha na kutathmini
- Uhariri
- Kuchapisha na kutoa mawaidha katika masuala ya lugha
- Kusawazisha viwango vya masomo
KUSULUHISHA MALALAMISHI
Wateja wetu wanashauriwa kuwasilisha mamalamishi yao kwa kufuata njia zifuatazo:
- Ana kwa ana
- Kupiga simu
- Baruapepe
- Barua
- Kisanduku cha mapendekezo
Idara itadumisha usiri wa mawasiliano yote baina yake na mteja
WAJIBU WA MTEJA
- Kupata huduma bora
- Kutagusana na idara kwa njia ya kunufaishana
- Kukosoa kwa nia ya kutaka kuboresha ubora wa huduma
- Kuleta majibu kuhusiana na ubora wa huduma zinazotolewa
- Kushiriki katika shughuli za idara
- Kupiga ripoti kwa haraka pale kasoro zinapobainika
- Kupeana taarifa za kutosha ili kuwezesha usaidizi kupatikana
KUJITOLEA KWETU KWA UTOAJI WA HUDUMA
- Wafanyikazi watawezeshwa kwa mujibu wa sera na sharia za Chuo Kikuu cha Nairobi
- Idara ya Kiswahili itabuni njia za kutolea malalamiko na kuulizia
- Usahihishaji utakamilika kwa muda wa majuma mawili kulingana na matakwa ya chuo
- Ufundishaji utaanza kwa wakati unaofaa
- Ufundishaji wote utatekelezwa kulingana na ratiba za Chuo Kikuu cha Nairobi
- Ufundishaji wote utalingana na silabasi mbalimbali zilizoidhinishwa na seneti
- Idara itahakikisha ya kwamba inakumbatia teknolojia
- Kesi zote za kinidhamu miongoni mwa wanafunzi zitakabidhiwa kwa mamalaka makuu ya kinadhamu kwa wakati unaofaa
- Ratiba za masomo zitawekwa wazi katika hadhara kwa wote kuona
- Tutahakikisha kuwepo kwa mawasiliano mema baina ya Idara ya Kiswahili, kitivo, shule na mamlaka makuu ya chuo
- Huduma zote katika idara zitaongozwa na sharia zilizowekwa na Chuo Kikuu cha Nairobi