AZIMIO LA IDARA LA DESEMBA 2 2020, KUHUSU UTUMIAJI WA KISWAHILI

Wahadhiri wa Idara ya Kiswahili

 

Wanaidara ya Kiswahili walipendekeza  kubadilishwa kwa sera chuoni. Idara ilikata kauli ya kuandika nyaraka zao zote kwa Kiswahili kwani ni lugha rasmi Kikatiba. Idara inaamini kuwa kumekuwa na uhamasisho wa kutosha kukihusu Kiswahili. Kama Idara, imeamua kutumia Kiswahili katika hali zote kazini. Ili kulisisitiza hili, Mwenyekiti Profesa Iribe alimyteua rasmi Dkt Hannah Mwaliwa kama kiongozi wa sera ya lugha Idarani. Jukumu lake muhimu ni kukumbusha mara kwa mara wanaidara kuhusu sera hii mpya. Kushadidia haya, Profesa Kineene Wamtiso aliunga mkono azimio hili kwa kusema haya “Wazo zuri sana. Wageni wajao chuoni kwetu na kutaka kufunzwa Kiswahili, hushangaa kwamba watu wengi huongea na kuwasiliana kwa Kiingereza  Hii ni moja ya sababu baadhi wao hubadili nia na kwenda Tanzania. Chuoni, kuna wahadhiri kutoka idara zingine, wanaovutiwa na Kiswahili sana. Lile ambalo unalipendekeza litawabadilisha nyoyo watu wengi. Pili, unajali maslahi ya sio wanaidara,  bali pia wote uwajuao na hili ni jambo zuri pia. Hivi karibuni tutakuwa na maporofesa wengi idarani. Jambo hili litawavutia wale wamejiunga nasi hivi karibu watamani nao kupanda juu. Hata sasa, tunaongoza, kwa kuwa na wahadhiri wengi, ambao wamepandishwa vyeo. Nina hakika kwamba waliokongamana katika kongamano letu la kimtandao  walivutiwa kwamba kuna wahadhiri wengi waliopandishwa vyeo kwetu. Fauka ya hayo, tulionyesha umoja mkubwa sana na takribani kila mtu akahusishwa kwa njia moja au nyingine. Yakini, haya yote yametokana na ushirikiano na utangamano mkubwa katika idara yetu. Kongole kwetu sote kwa kuwa na umoja huu”

Hotuba ya mwenyekiti wa idara ya kiswahili Prof. Iribe Mwangi kwenye webina ya kimataifa iliyoandaliwa na idara ya Kiswahili, alikuwa na ombi kwa niaba ya Idara kwamba Chuo Kikuu cha Nairobi, kama ilivyo kawaida yake kuongoza katika ubadilishaji wa sera ya lugha Chuoni. Kiwe Chuo Kikuu cha kwanza nchini (labda hata ulimwenguni) kufanya mahafali (graduation ceremony) yake kwa Kiswahili. Tutafurahia sana hili elikifanyika na kama Idara tutakuwa radhi kusaidia.