Latest News & Announcements

Prof. Olali, Prof.Mogambi, Prof.Chimera, Prof.Muaka, Mombasa

Waziri, katika Wizara ya Utalii, Wanyamapori na Turathi, Mhe. Peninah Malonza, leo hii amejumuika na wakaazi wa Mombasa ili kuadhimisha Siku ya Kiswahili duniani.

Maadhimisho hayo yalianza na msafara ulioanzia Mapemebeni, na kuelekea hadi kituo cha Utamaduni wa Waswahili, pembezoni Ngomeni.

Novemba 23, 2021, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), liliteua Julai 7 kuwa siku rasmi ya kuadhimisha lugha ya Kiswahili duniani, hivyo basi, kuzifanya sherehe hizo kua za pili tangu uteuzi huo.

Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani 2023: Amani na Ustawi

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani tarehe Saba, Mwezi Julai 2023 ni “Kiswahili kwa Amani na Ustawi.” Lengo kuu la maadhimisho haya ni kusaidia kunogesha matumizi ya lugha ya Kiswahili kama nguvu ya amani, ustawi na maendeleo endelevu ya binadamu sanjari na mchakato wa kuimarisha tamaduni mbalimbali. Siku hii ilianzishwa na UNESCO tarehe 23 Novemba 2021 na kuanza kuadhimishwa tarehe 7 Julai 2022. Leo tunayo Historia ya Kiswahili.

Idara ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Nairobi kilishiriki katika hafla hiyo kikamilifu.