Bunge la kitaifa lajadili uwepo wa baraza la kiswahili

Wabunge wanasema ni wakati kwa Kenya kubuni baraza la kitaifa la kiswahili, kusaidia kuipa lugha hii hadhi inayostahiki. Wabunge waliokuwa wakichangia hoja ya mbunge wa Kamukunji Yusuf Hassan walisema kuwa, kuimarishwa kwa utumizi na hadhi ya kiswahili kutasaidia kuimarisha utangamano zaidi, sio tu hapa nchini na kanda ya Afrika Mashariki, bali pia dunia nzima ambapo lugha hii inaenziwa. Hoja hii ya kamati ya utamaduni na utalii likiwataka wabunge kuanzisha rasmi baraza la kiswahili la Kenya na kuzindua mikakati, mbinu na sera mahususi zinazohitajika kukuza na kuendeleza lugha ya kiswahili