KUBIDHAISHA KISWAHILI

Bi Betty Maina, C.B.S., Waziri wa Viwanda, Biashara na Ukuaji wa Biashara ya Jamhuri ya Kenya

Nchi ya Kenya imekuwa mbioni kujiandaa kibiashara katika siku za usoni. Ari ya kujiandaa kibiashara imechocewa na mambo mawili muhimu: Kwanza, Sheria ya Ukuaji na Fursa Barani Afrika (AGOA), mpango wa upendeleo, unafika kikomo mwisho wa mwaka 2025.  Kwa sababu hii, nchi ya Kenya inapanga mikakati yake ya biashara baada ya 2025. Hata hivyo, mazungumzo yake yanakaribisha nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Pili, ni kujiondoa kwa Uingereza kutoka kwa Jumuiya ya Ulaya (Brexit). Nchi ya Kenya (na Jumuiya ya Afrika Mashariki) inapanga namna ambavyo itaendeleza biashara yake na Uingereza baada ya mchakato huo. Kwa sababu hityo, kumekuwa na mazungumzo baina ya Kenya na Uingereza na kwa upande wa Kenya, mazungumzo hayo yanaongozwa na Wizara Viwanda, Biashara na Maendeleo ya Kibiashara Bi. Betty Maina na Katibu Mkuu wa Biashara na Maendeleo ya Kibiashara Balozi Johnso Weru.

Swali la kujiuliza ni je, Kiswahili kinaweza kubidhaishwa na kukuzwa kibiashara? Kiswahili kinaweza kunufaika vipi kutoka kwa majidiliano kama haya? Kwa kuwa mazungumzo haswa yanalenga Jumuiya ya Afrika Mashariki, ni kwa vipi wananchi wa nchi hizi wanaweza kutumia Kiswahili kama biashara?

Ili kuelewa haya, Idara itakuwa ikitoa ruwaza za masuala mbalimbali yanayohusu mikataba ya biashara na inatarajiwa kuwa makala hayo yatasaidia katika kubainisha nafasi ya Kiswahili katika biashara na kuona ni kwa vipi kinaweza kuwanufaisha watumizi.

Hapa chini ni taarifa ya pamoja inayotolewa na Bi. Betty Maina, Katibu wa Wizara, Wizara ya Viwanda, Biashara na Ukuaji wa Biashara na Mhe.  James Duddridge, Mbunge, Waziri wa Afrika kutoka Uingereza, kufuatia mkutano kuhusu Jukwaa la Maendeleo ya Kiuchumi wa Uingereza na Kenya.

 

Taarifa ya pamoja inayotolewa na Bi. Betty Maina, Katibu wa Wizara, Wizara ya Viwanda, Biashara na Ukuaji wa Biashara na Mhe.  James Duddridge, Mbunge, Waziri wa Afrika kutoka Uingereza, kufuatia mkutano kuhusu Jukwaa la Maendeleo ya Kiuchumi wa Uingereza na Kenya

Kenya na Uingereza zilifanya Mkutano wao wa pili kuhusu Jukwaa la Maendeleo ya Kiuchumi kupitia mtandao mnano tarehe 13 Novemba 2020.

Jukwaa hili liliongozwa kwa pamoja na Bi Betty Maina, C.B.S., Waziri wa Viwanda, Biashara na Ukuaji wa Biashara ya Jamhuri ya Kenya, na Mhe. James Duddridge, Mbenge, Waziri wa Afrika katika Ofisi ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo ya Uingereza.

Nguzo ya Ustawi wa pamoja wa Uingereza na Kenya ya Mkakati wa Ushirikiano inaeleza kuwa Uingereza na Kenya zitashirikiana kukuza ustawi wa pamoja, kukuza ukuaji wa uchumi na kuunda ajira na kujenga uhusiano mzuri wa kibiashara na uwekezaji. Jukwaa la Maendeleo ya Kiuchumi ni mkakati wa utoaji wa nguzo ya Ustawi wa Pamoja. Jukwaa lilikubaliana kuhusu Mpango wa Utekelezaji wa Ustawi wa Pamoja ambao unafafanua mipango ya kutoa ahadi za pamoja chini ya Ushirikiano wa Kimkakati baina ya Kenya na Uingereza.

Makubaliano katika Kanuni ya Mkataba wa Kibiashara baina ya Uingereza na Kenya

Jukwaa lilikaribisha Makubaliano katika Kanuni ya Mkataba wa Kibiashara baina ya Uingereza na Kenya, ulioridhiwa tarehe 3 Novemba 2020. Mkatabwa utakapoanza kutumika, kama inavyotarajiwa, mwishoni mwa 2020 utalinda ufikiaji wa muda mrefu bila ushuru na kwa upendeleo kwa Uingereza kwa mauzo ya nje ya Kenya na jumla ya biashara na mipangilio ya uchumi. Makubaliano haya yanatokana na hati ya Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya na Mataifa ulioridhiwa na Washriki wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanaweza kujiunga nao. Hati hiyo inafanyiwa uchunguzi wa kisheria na baadaye itaandaliwa ili ilitiwe saini katika wiki zijazo kabla ya kuwekwa katika michakato ya kitaifa, ikijumuisha Mabunge, ili kukamilisha michakato ya kuridhiwa.

Mada nyingine za majadiliano

Jukwaa hili lilitambua mkabilio wa haraka na madhubuti wa Kenya kwa janga la COVID-19, na kuahidi msaada wa Uingereza kusaidia kudumisha mifumo ya usambazaji wa bidhaa, kufungua biashara kwa njia salama wakati wa COVID-19, na kusaidia kuhifadhi uwekezaji nchini Kenya. Uingereza imejitolea kusaidia Kenya kuvutia uwekezaji na kukuza sekta muhimu, pamoja na kuchochea uwekezaji wa hatua za mapema ("uwekezaji binafsi") katika biashara zinazoanza.         

Jukwaa lilikaribisha kujitolea kwa pamoja kwa Uingereza na Kenya kuboresha mazingira ya kibiashara na uwekezaji. Wajumbe wote walikubaliana kuhusu umuhimu wa kushirikiana zaidi na mashirika ya kibiashara kujadili mitazamo yao kuhusu hatua ambazo zitaboresha mazingira ya kibiashara. Jukwaa lilikagua baadhi ya changamoto zinazoripotiwa kawaida zinazokabili wafanyabiashara wa Uingereza wanaofanya kazi nchini Kenya na kukubali kuanzisha kwa pamoja mifumo, kwa fursa ya mapema zaidi, kushughulikia changamoto hizi na kupata suluhisho.

Jukwaa lilikaribisha uteuzi wa Jopokazi la Pamoja la Utafutaji wa Fedha kutoka Sekta Binafsi na jukumu lake katika kupeleka mbele nia yetu ya kuongeza fursa za uwekezaji za Uingereza na Kenya, kutafuta mtaji, na kujenga ushirikiano mpya na Jiji la London Serikali zote mbili zilijitolea kupeleka mbele kasi haii katika Kituo cha Fedha cha Kimataifa cha Nairobi, pamoja na kuimarisha uhusiano kati ya vituo vya kifedha vya London na Nairobi. Jukwaa limejitolea kuendeleza ushirikiano wetu madhubuti wa kutafuta fedha za kusaidia hatua za hali ya hewa na kukaribisha maendeleo ya Serikali ya Kenya kuhusu mpango uliowekwa kwa kutoa dhamana huru ya kijani na uongozi unaoendelea katika kanda wa kuongezeka kwa fedha za kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa.

Jukwaa lilitambua maendeleo mazuri yanayofanyika kwenye mradi wa  Reli la Jili la Nairobi, liliitambuliwa kama sehemu muhimu ya ushirikiano wa kimkakati baina ya Uingereza na Kenya na kukaribisha kujitolea kwa Uingereza kwa awamu ya pili ya msaada.

Katika kuhitimisha, Jukwaa hili lilitambua manufaa ya uhusiano wa kiuchumi baina ya Kenya na Uingereza, na wajumbe wote walijitolea kufanya kazi pamoja ili kuendelea kujenga ustawi wa pande zote. Jukwaa hili lilithibitisha kujitolea kutoka kwa Serikali za Kenya na Uingereza kufanya mikutano ya ufuatilizi kila baada ya miezi sita kukagua maendeleo kuhusu ahadi za Ushirikiano wa Kimkakati na kujadili jinsi ya kukuza ukuaji wa kiuchumi na uundaji wa ajira, na pia kujenga uhusiano mzuri wa kibiashara na uwekezaji.