MKUTANO WA IDARA YA KISWAHILI ULIOFANYIKA KUPITIA MTANDAO TAREHE 30 AGOSTI 2020

Huu ni  mkutano wa pili wa idara kufanyika kupitia mtandao na wa kufaulisha mno.

Agenda za mkutano;

  1. Mawasiliano kutoka kwa Mwenyekiti
  2. Maendelezo ya mitihani ya Bed, BA na MA
  3. Mikakati kuhusu mitihani kuendelea mbele
  4. Mawasilisho na utahini wa kazi za uzamili na uzamivu
  5. Mgao wa kozi Kuanzia Muhula Ujao  
  6. Usawazishaji Mitihani ( Moderation of Exams)
  7. Masuala Mengineyo

Mwenyekiti aliwashukuru wana idara kwa jitahada zao kutimiza mambo ya Chuo kwa ushirikiano. Aliwahimiza wanaidara kuendelea na moyo huo kwani hangependa mwanaidara yoyote kutatizika ikiwa hatatimiza mahitaji ya Chuo. Haya pamoja na mengine mengi yalionyesha jitihada walimu wanaweka katika ufundishaji na utahini wa mitihani mtandaoni licha ya kukumbwa na changamoto si haba.

Walimu waliahidi kushirikiana ili kuafiki malengo ya idara pamoja na chuo.

Comments

Submitted byjudynyamweya16 on Thu, 07/30/2020 - 21:56

Idadi kubwa ya wanaidara waliweza kuhudhuria mkutano wa leo. Hii ni ishara kuwa, kuna matumaini ya kushinda' changamoto za kimtandao. Kongole wanaidara