Prof Rayya aliwasilisha kwenye jukwaa la kimataifa Ujerumani kwenye Baraza la Kiswahili la Berlin (BALAKI-BE) la tarehe 11 Disemba 2023
Katika wasilisho hili Rayya Timammy aliyajadili masuala yanayolingana na matumizi ya madawa ya kulevya katika jamii ya Waswahili wa pwani ya Kenya. Swala la matumizi ya madawa ya kulevya au mihadharati ni donda sugu katika jamii mbalimbali ulimwenguni. Vijana wengi ambao wanatarajiwa kuwa tegemeo la jamii wameathirika na madawa ya kulevya na hivyo kuwa mzigo kwa familia na jamii kwa jumla. Kwa kuwa fasihi husemwa kuwa ni kioo cha jamii, inatarajiwa kudhihirisha hili. Ni muhali kwa mwandishi wa kifasihi kujitenga na hali halisi zinazoikumba jamii anayoiandikia kwa vile fasihi ni zao la jamii na hivyo inaathiriwa na shughuli za jamii. Katika wasilisho hili, Timammy aliangazia jinsi ushairi wa Kiswahili unavyolishughulikia suala hili, hasa akijikita katika ushairi wa pwani ya Kenya. Zaidi atajifunga na kazi mbili za ‘Utenzi wa Mikhadharati’ wa Mahmoud Abdulkadir hapo akiligusia shairi la ‘Madawa ya Kulevya’ la Alamin Somo.
- Log in to post comments