Webina ya Idara ya Kiswahili

Kama sehemu ya maadhimisho ya jubilee ya miaka hamsini, idara ya Kiswahili kupitia kamati andalizi  imeandaa Webina yenye mada kuu; Kiswahili Ulimwenguni.

Hafla hiyo itafanyika Desemba 2, 2020 kwanzia 2.00 mchana hadi 5.30 jioni. Mfunguzi wa hafla hiyo ni Makamu mkuu wa Chuo, Profesa Stephen Kiama.  Makala Elekezi yatajadiliwa na  Prof. Mwenda Ntarangwe, kutoka Tume ya Elimu ya Vyuo Vikuu. Mwasilishaji wa makala maalum ni Prof. Ngugi wa Thiong’o, Chuo Kikuu cha California, Irvine.

Wawasilishi wengine ni pamoja na Prof. Lisanza Muaka (Howard), Prof. Kineene (Nairobi), Yuning Shen (Zhejiang)

Mratibu wa Webina ni Prof. Tom Olali, Idara ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Nairobi.

Maelezo zaidi yamo katika kipeperushi kilichoambatanishwa.