Prof. Iribe Mwangi, mwalimu wa Kiswahili ni miongoni mwa Wakenya 460 waliotuzwa na Rais William Ruto katika sherehe za Kitaifa za 59 za jamuhuri.
Profesa Iribe ni ni mwenyekiti wa Idara ya Kiswahili chuo kikuu cha Nairobi. Aliweza kutunukiwa tuzo ya Head of State Commendation (HSC) kwa mchango wake katika makuzina maendeleo ya Kiswahili ambayo yameathiri sera ya lugha nchini Kenya.
Profesa Iribe ni mtetezi wa Kiswahili katika vyombo vya habari ambapo huangazia masuala tofauti kuhusu maendeleo ya Kiswahili katika ukanda wa Afrika Mashariki na ulimwenguni. Mtaalamu huyu ambaye amewalea wasomi wengine chipukizi ana machapisho yasiyopungua 80 yakiwemo vitabu, sura kwenye vitabu na makala katika majarida ya kitaaluma.
- Log in to post comments