Mradi huu uliasisiwa mwaka 2020 chini ya ufadhili wa Carnegie African Diaspora Fellowship Program (CADFP). Tuzo ya CADFP ilimwezesha Profesa Mungai Mutonya wa Chuo Kikuu cha Washington University Mjini St. Louis na mwana-CADFP mwenzake, Profesa Iribe Mwangi, aliye Mwenyekiti wa Idara ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Nairobi (UoN), kubuni mikakati mwafaka ya kiutafiti inayoendeleza mradi hadi sasa. Tuzo ya CADFP 2022 iliongezea ushirikiano wa kiutafiti na kuwezesha mradi kupiga hatua muhimu.
Lengo kuu la mradi huu ni kusawiri kwa njia ya ramani, mtagusano changamana wa lugha unaotokana na uhamiaji kutoka nchi mbalimbali za Afrika. Aidha, mradi unaangazia hali changamana ya lugha jijini Nairobi na uhalisi wa kimawasiliano katika jiji hili kuu la Afrika Mashariki.
Tovuti hii inalenga jumuiya zifuatazo:
- Wenyeji wa Nairobi wanaopenda kuyafahamu mazingira yao
- Wenyeji waliohamia Nairobi kutoka nchi mbalimbali na waliokubali kuhojiwa
- Wenyeji wa Nairobi walio na ukarimu wa kuwakaribisha na kuishi kwa amani na wenyeji wapya walio na lugha na asili tofauti.
- Wenyeji kutoka sehemu mbalimbali za Kenya, Afrika, waliohamia Nairobi kusoma na kujitafutia riziki.
Mradi huu unatambua mchango wasomi, watafiti, walimu, wanafunzi, waandishi habari, na wote wanaoangazia masiala ya matumizi ya lugha jijini Nairobi. https://mmutonya9.wixsite.com/lughazanairobi
- Log in to post comments