Kutoka kushoto ni Prof. Iribe wa Mwangi, Prof. Kyalo Wadi Wamitila, Prof. Rayya Timmamy, Dkt. Evans Mbuthia na Bi. Mary Ndung'u wakati wa Kongamano la Nne la Kimataifa la Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (Chaukidu) lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar, kisiwani Unguja, mwezi Disemba 2018.
Wanafunzi wa Idara ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Nairobi wanaosomea kozi ya CLK 404: Kiswahili Oral Literature and Culture chini ya usimamizi wa Prof.Tom Olali wakipata mafunzo maalum ya moja kwa moja ya jinsi ya kutayarisha biriani ya nyama. Hapa wanaonyeshwa hatua hizo na Bi. Lulu Ali, Amira Msellem na Dia Chuda kule Kibokoni, Mji wa Kale.