0
Webina liyoandaliwa na Idara ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Nairobi Kusherehekea Miaka 50 ya Jubilee
Siku Jumatano tarehe 2, Disemba, 2020, Idara ya Kiswahili kupitia kamati andalizi, iliandaa webina kusherehekea miaka 50 tangu Chuo Kikuu cha Nairobi kilipoanzishwa rasmi. Kauli Mbiu ya webina ilikuwa, “Kiswahili Ulimwenguni.”