Kama sehemu ya maadhimisho ya jubilee ya miaka hamsini, idara ya Kiswahili kupitia kamati andalizi imeandaa Webina yenye mada kuu; Kiswahili Ulimwenguni.
Hafla hiyo itafanyika Desemba 2, 2020 kwanzia 2.00 mchana hadi 5.30 jioni. Mfunguzi wa hafla hiyo ni Makamu mkuu wa Chuo, Profesa Stephen Kiama. Makala Elekezi yatajadiliwa na Prof. Mwenda Ntarangwe, kutoka Tume ya Elimu ya Vyuo Vikuu. Mwasilishaji wa makala maalum ni Prof. Ngugi wa Thiong’o, Chuo Kikuu cha California, Irvine.
Nchi ya Kenya imekuwa mbioni kujiandaa kibiashara katika siku za usoni. Ari ya kujiandaa kibiashara imechocewa na mambo mawili muhimu: Kwanza, Sheria ya Ukuaji na Fursa Barani Afrika (AGOA), mpango wa upendeleo, unafika kikomo mwisho wa mwaka 2025. Kwa sababu hii, nchi ya Kenya inapanga mikakati yake ya biashara baada ya 2025. Hata hivyo, mazungumzo yake yanakaribisha nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki.