Binadamu anaweza kuchagua kuwa mwema ama mui kutegemea hulka yake. Hata hivyo, mazingira pia huwa na athari katika kukuza hulka ya mtu. Ni uteuzi
Mradi huu uliasisiwa mwaka 2020 chini ya ufadhili wa Carnegie African Diaspora Fellowship Program (CADFP). Tuzo ya CADFP ilimwezesha Profesa Mungai Mutonya wa Chuo Kikuu cha Washington University Mjini St. Louis na mwana-CADFP mwenzake, Profesa Iribe Mwangi, aliye Mwenyekiti wa Idara ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Nairobi (UoN), kubuni mikakati mwafaka ya kiutafiti inayoendeleza mradi hadi sasa. Tuzo ya CADFP 2022 iliongezea ushirikiano wa kiutafiti na kuwezesha mradi kupiga hatua muhimu.