MKUTANO WA IDARA YA KISWAHILI ULIOFANYIKA KUPITIA MTANDAO TAREHE 6 APRILI 2020

Huu ni mkutano wa kwanza uliofanyika kupitia mtandaoni. Ajenda kuu zilikuwa ; mawasiliano kutoka kwa Mwenyekiti; Makaribisho ya walimu wapya;  Livu ya mwaka, Utahini wa tasnifu za uzamifu; Usimamizi wa tasnifu za uzamili na uzamifu; Ufundishaji wa wanafunzi wa MA, BA na BED na maswala mengineyo.

Hoja kuu kutoka kwa mkutano huo ni pamoja na; wwenyekiti kuhimiza walimu kutumia mtandao kuwafikia wanafunzi wanaofundishwa kutumia njia mbalimbali zilizomo k.v Zoom, WhatsApp na kadhalika.

Pili,ukaribisho wa walimu wapya kwenye Idara ya Kiswahili na kumpa kila mmoja nafasi ya kujitambulisha kwa wahadhiri wengine. Walimu hao ni:
a. Mwalimu Samson Ongarora: ana ujuzu katika Fasihi ya Kiswahili,
b. Mwalimu Andrew Ignitious Watuha: ana ujuzi katika Isimu ya Kiswahili, na
c. Mwalimu Judy Onyancha: ana ujuzi katika Historia na Maendeleo ya Kiswahili

Mwenyekiti aidha  aliwashauri walimu walio na malibikizi ya siku za livu kuchukua livu katika kipindi hiki, pia, kwa hiari.