Wana idara

KONGAMANO LA 6 LA KIMATAIFA, CHUO KIKUU CHA PWANI KILIFI, KENYA

Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) kimeandaa kongamano la 6 la kimataifa katika Chuo Kikuu cha Pwani Kilifi, Kenya mnamo tarehe 15-17 Dis. 2020

Mda wa makataa ya ikisiri uliongezwa hadi Tarehe 30 Juni, 2020. Wapenzi na wasomi wa Kiswahili wanaombwa kutuma ikisiri kabla au kufikia tarehe ya makataa.

Taarifa zaidi kuhusu CHAUKIDU zimo katika kiambatisho.

 

MKUTANO WA IDARA YA KISWAHILI ULIOFANYIKA KUPITIA MTANDAO TAREHE 6 APRILI 2020

Huu ni mkutano wa kwanza uliofanyika kupitia mtandaoni. Ajenda kuu zilikuwa ; mawasiliano kutoka kwa Mwenyekiti; Makaribisho ya walimu wapya;  Livu ya mwaka, Utahini wa tasnifu za uzamifu; Usimamizi wa tasnifu za uzamili na uzamifu; Ufundishaji wa wanafunzi wa MA, BA na BED na maswala mengineyo.

Hoja kuu kutoka kwa mkutano huo ni pamoja na; wwenyekiti kuhimiza walimu kutumia mtandao kuwafikia wanafunzi wanaofundishwa kutumia njia mbalimbali zilizomo k.v Zoom, WhatsApp na kadhalika.