UoN @50

Kuanzia mwezi Juni 2020 hadi Juni 2021, Chuo Kikuu cha Nairobi kinaadhimisha miaka 50 tangu kuasisiwa kwake. Kumekuwa na shughuli nyingi hasa webina za kiusomi ambazo zimekuwa zikiendelea na zitaendelea hadi Juni 2021. Idara ya Kiswahili tayari imekwishaandaa webina iliyokuwa na kaulimbiu ya “Kiswahili Ulimwenguni.” Hata hivyo, kilele cha sherehe hizi kitakuwa Alhamisi tarehe 10 Desemba 2020 kuanzia saa nane alasiri.

Sherehe za Mahafali ya 64, Chuo Kikuu cha Nairobi - Ijumaa, Desemba 11, 2020

Sherehe hizi zitafanyika mnamo tarehe 11 Desemba kuanzia saa mbili asubuhi. Sherehe hizi zitafanyika kupitia mtandao kutokana na janga la Korona. Kati ya watakaofuzu ni wazamifu 66. Hii ni sherehe ya pili kufanyika kwa njia ya mtandao huku ya kwanza ikifanyika tarehe 25 Septemba, 2020. Ndaki yetu ya Insia na Sayanzi za Jamii ndiyo itakayokuwa na washiriki wengi kabisa.