MKUTANO WA IDARA YA KISWAHILI ULIOFANYIKA KUPITIA MTANDAO TAREHE 6 APRILI 2020
Huu ni mkutano wa kwanza uliofanyika kupitia mtandaoni. Ajenda kuu zilikuwa ; mawasiliano kutoka kwa Mwenyekiti; Makaribisho ya walimu wapya; Livu ya mwaka, Utahini wa tasnifu za uzamifu; Usimamizi wa tasnifu za uzamili na uzamifu; Ufundishaji wa wanafunzi wa MA, BA na BED na maswala mengineyo.
Hoja kuu kutoka kwa mkutano huo ni pamoja na; wwenyekiti kuhimiza walimu kutumia mtandao kuwafikia wanafunzi wanaofundishwa kutumia njia mbalimbali zilizomo k.v Zoom, WhatsApp na kadhalika.