Latest News & Announcements

UoN @50

Kuanzia mwezi Juni 2020 hadi Juni 2021, Chuo Kikuu cha Nairobi kinaadhimisha miaka 50 tangu kuasisiwa kwake. Kumekuwa na shughuli nyingi hasa webina za kiusomi ambazo zimekuwa zikiendelea na zitaendelea hadi Juni 2021. Idara ya Kiswahili tayari imekwishaandaa webina iliyokuwa na kaulimbiu ya “Kiswahili Ulimwenguni.” Hata hivyo, kilele cha sherehe hizi kitakuwa Alhamisi tarehe 10 Desemba 2020 kuanzia saa nane alasiri.

Sherehe za Mahafali ya 64, Chuo Kikuu cha Nairobi - Ijumaa, Desemba 11, 2020

Sherehe hizi zitafanyika mnamo tarehe 11 Desemba kuanzia saa mbili asubuhi. Sherehe hizi zitafanyika kupitia mtandao kutokana na janga la Korona. Kati ya watakaofuzu ni wazamifu 66. Hii ni sherehe ya pili kufanyika kwa njia ya mtandao huku ya kwanza ikifanyika tarehe 25 Septemba, 2020. Ndaki yetu ya Insia na Sayanzi za Jamii ndiyo itakayokuwa na washiriki wengi kabisa.

Webina ya Idara ya Kiswahili

Kama sehemu ya maadhimisho ya jubilee ya miaka hamsini, idara ya Kiswahili kupitia kamati andalizi  imeandaa Webina yenye mada kuu; Kiswahili Ulimwenguni.

Hafla hiyo itafanyika Desemba 2, 2020 kwanzia 2.00 mchana hadi 5.30 jioni. Mfunguzi wa hafla hiyo ni Makamu mkuu wa Chuo, Profesa Stephen Kiama.  Makala Elekezi yatajadiliwa na  Prof. Mwenda Ntarangwe, kutoka Tume ya Elimu ya Vyuo Vikuu. Mwasilishaji wa makala maalum ni Prof. Ngugi wa Thiong’o, Chuo Kikuu cha California, Irvine.

KUBIDHAISHA KISWAHILI

Nchi ya Kenya imekuwa mbioni kujiandaa kibiashara katika siku za usoni. Ari ya kujiandaa kibiashara imechocewa na mambo mawili muhimu: Kwanza, Sheria ya Ukuaji na Fursa Barani Afrika (AGOA), mpango wa upendeleo, unafika kikomo mwisho wa mwaka 2025.  Kwa sababu hii, nchi ya Kenya inapanga mikakati yake ya biashara baada ya 2025. Hata hivyo, mazungumzo yake yanakaribisha nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki.