Latest News & Announcements

Nairobi Public Speaking High Tea

 Wanafunzi wetu watatu wa CLK 401: Public Speaking and Speech Writing in Kiswahili Maena, Abigael Malesi na Ruth Kamene walipata ufadhili wa kuhudhuria warsha ya "Speaking Confidence" katika "Nairobi Oublic Speaking High Tea" pale Gem Suites, Riverside Drive tarehe 1 Desemba, 2023.Kila mshiriki alilipa 45k.Prof.Tom Olali aliweza kupata ufadhili wa wanafunzi 10.

Lugha za Nairobi

Mradi huu uliasisiwa mwaka 2020 chini ya ufadhili wa Carnegie African Diaspora Fellowship Program (CADFP). Tuzo ya CADFP ilimwezesha Profesa Mungai Mutonya wa Chuo Kikuu cha Washington University Mjini St. Louis na mwana-CADFP mwenzake, Profesa Iribe Mwangi, aliye Mwenyekiti wa Idara ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Nairobi (UoN), kubuni mikakati mwafaka ya kiutafiti inayoendeleza mradi hadi sasa. Tuzo ya CADFP 2022 iliongezea ushirikiano wa kiutafiti na kuwezesha mradi kupiga hatua muhimu.